Shamba Darasa
Madhumuni ya Shamba Darasa letu ni kusaidia wafugaji wachanga/wapya na hata wazoefu kupata uzoefu zaidi.Tumedhamiria kutoa elimu kwa gharama nafuu kwa jamii nzima ili kuleta tija katika ufugaji.Tunaamini na kushauri kabla mtu kuanza ufugaji basi vyema yeye au watu watakao simamia mradi wapate fursa ya kujifunza kwa vitendo ili kuwa na uelewa mpana.Mafunzo haya yataleta tija kwani yataongeza nafasi ya mradi kufanikiwa.
Shamba Darasa letu ni la siku 10 mpaka 14 na zinaweza ongezwa kwa mlengwa kuomba,Tunachukua wamafunzi sita (6) mpaka nane (8) kwa wakati mmoja.Wanafunzi au walengwa wanaweza lala shambani ambapo watapatiwa malazi na vyakula.Wataingia darasani kupata mafunzo na shambani yaani kwenye mifugo kujifunza kwa vitendo.Tunamkufunzi ambae ni Daktari wa Mifugo na wakufunzi wa vitendo kwa uzoefu.Gharama zatu ni nafuu sana.Shamba darasa letu linahushisha ufugaji wa Nguruwe kibiashara,Kuku,Mabata na Ndege wengine pamoja na samaki.Mshiriki atapata nafasi ya kujifunza ufugaji wa mfugo anaokusudia kufuga kuanzia hatua za awali mpaka mwisho.Karibuni sana